Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA-SIASA-HAKI

Mwanamuziki maarufu na Mbunge Bobi Wine aamua kurudi Kampala

Mwanamuziki maarufu na Mbunge wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina la Bobi Wine, anasema kuwa ameamua kurudi nyumbani baada ya matibabu nchini Marekani, licha ya kushtakiwa kosa la uhaini.

Mwanamuziki maarufu na Mbunge Robert Kyagulanyi, anayefahamoka kwa jina la Bobi Wine, katika mkutano na waandishi wa habari na wakili wake huko Washington, DC, Septemba 6, 2018.
Mwanamuziki maarufu na Mbunge Robert Kyagulanyi, anayefahamoka kwa jina la Bobi Wine, katika mkutano na waandishi wa habari na wakili wake huko Washington, DC, Septemba 6, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kyagulanyi, mwenye umri wa miaka 36, ameibuka kama msemaji wa vijana wa Uganda na mkosoaji mkubwa wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, ambaye yuko madarakani tangu mwaka 1986.

Alihukumiwa, pamoja na watuhumiwa wengine 32 wa kufuatia kile kilichoelezwa kuwa alishiriki katika vurugu za uchaguzi mdogo ambapo gari la msafara wa Rais lilishambuliwa kwa mawe Agosti 14, 2018.

Bobi Wine anakabiliwa na makosa ya uhaini, kufuatia tukio la kushambuliwa kwa mawe gari la Rais Yoweri Kaguta Museveni. Aliachiliwa kwa dhamana kutoka kizuizini alikokuwa akishikiliwa huko Gulu.

Wakati wa vurugu hizo, dereva wa Bobi Wine aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi na yeye mwenyewe alikamatwa, na kusababisha maandamano makubwa nje na ndaji ya mji mkuu wa Uganda, Kampala, maandamano ambayo yalivunjwa kikatili na vikosi vya ulinzi na usalama.

"Ninataka kurudi nyumbani, nataka kuendelea kutolea wito Waganda wote kupigana kwa ajili ya kile wanachoamini," amesema huko Washington, ambako anapata matibabu ya majeraha ambayo anaamini yalisababishwa na unyanyasaji na mateso alipokua akizuiliwa.

Serikali ya Uganda imefutilia mbali shutma hizo.

"Ninaweza kwenda jela, kuna hatari ni hukumiwe kifo, lakini pia ninaweza kuuawa," amsema mwanasiasa huyo wa upinzani, aliyechaguliwa kuwa Mbunge mnamo mwaka 2017 na ambaye alizungumza kwa mara ya kwanza tangu aliwasili nchini Marekani mapema mwezi Septemba.

Mwanasheria wake, Robert Amsterdam, aliomba Marekani kulaani "vitendo vya kihalifu na ukiukaji wa kila siku wa haki za binadamu" na vikosi vya usalama vya Uganda.

"Silaha na vifaa vya kijeshi vya Marekani hutumiwa kwa kutesa Waganda," mwanasheria amewaambia waandishi wa habari, akitoa wito kwa Marekani "kusitishwa mara moja kufadhili jeshi la Uganda."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.