Pata taarifa kuu
KENYA-MAREKANI-USHIRIKIANO-UCHUMI-USALAMA

Uhuru Kenyatta kukutana na Donald Trump White House

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajia kukutana Jumatatu hii Agosti 27 na mwenyeji wake rais wa Marekani Donald Trump kwenye ikulu ya White House.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atapokelewa katika White House na mwenyeji wake rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atapokelewa katika White House na mwenyeji wake rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Rais Kenyatta aliwasili tangu Jumamosi, Agosti 25 mjini Washington kwa ziara ya siku nne nchini Marekani kwa mwaliko wa Donald Trump. Huu ni mkutano wa kwanza kati ya rais wa Kenyana mwenyeji wake rais wa Marekani Donald Trump. Hii ni mara ya pili rais wa Marekani Donald Trump kumualika kiongozi kutoka Afrika, baada ya Muhammadu Buhari wa Nigeria mwezi Aprili 2018. Rais Kenyata na mwenyeji wake watajadili kuhusu ushirikiano wa kikanda na masuala ya usalama, lakini pia biashara na uwekezaji.

Wakati wa mkutano wao Jumatatu wiki hii katika ikulu ya White House, Uhuru Kenyatta na Donald Trump watajadili kuhusu masuala ya usalama, ikiwa ni pamoja na mchakato wa amani nchini Sudan Kusini, wakati ambapo mazungumzo yanaendelea huko Khartoum kati ya serikali na waasi chini ya upatanishi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD).

Lakini pia wawaili hao watajadili kuhusu vita dhidi ya ugaidi. Kenya ni mshirika wa karibu wa Marekani katika vita dhidi ya kundi la al-Shabab lenye mafungamano na al-Qaeda nchini Somalia. Lakini tangu uchaguzi wa Donald Trump, Marekani imeongeza uwepo wake nchini Kenya na mashambulizi ya angani dhidi ya kundi hili la wanamgambo wa Kiislam.

Mikataba ya kiuchumi

Kwa mujibu wa Njeru Githae, balozi wa Kenya huko Washington, mkutano huo kwanza kabisa una malengo ya kiuchumi. "Rasimu kadhaa za mikataba zinaendelea kuzungumziwa na tuna imani kuwa itasainiwa," amesema.

Kenya inataka kuongeza mauzo yake nchini Marekani kupitia taasisi ya AGOA, sheria juu ya ukuaji na maendeleo katika Afrika, na hata kuanza majadiliano juu ya mikataba ya baada ya AGOA ili kuwezesha upatikanaji wa Soko la Marekani kwa bidhaa za Kenya.

Uhuru Kenyatta pia anataka kuwatolea wito wafanyabiashara wa kubwa wa Marekani kuwekeza nchini Kenya. Atakutana na wawakilishi wa wabiashara Jumatatu hii asubuhi. Fursa kwa rais wa Kenya kutafuta msaada na ufadhili kwa maendeleo ya sekta ya viwanda nchini Kenya, mojawapo ya nguzo nne za mpango wake kwa nchi.

♦ Nchi mbili zenye uhusiano wa karibu

"Mkutano huu utasisitiza uhusiano kati ya Marekani na Kenya kama washirika katika kusimamia amani na utulivu barani Afrika na eneo la Pacific," ikulu ya White House imebaini katika taaria yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.