Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-USALAMA

Makundi hasimu kutia saini mkataba wa mwisho Jumatatu Sudan Kusini

Mkataba wa mwisho wa amani nchini Sudan Kusini unatarajiwa kutiwa saini Jumatatu ijayo, jijini Khartoum nchini Sudan. Mkataba huu unaeleza kuachiliwa huru kwa wafungwa, utoaji wa misaada ya kibinadamu na kuundwa kwa serikali ya mpito ndani ya miezi minne.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (katikati) anashikilia mkono wa hasimu wake Riek Machar kabla ya kutia saini makubaliano huko Khartoum Agosti 5, 2018.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (katikati) anashikilia mkono wa hasimu wake Riek Machar kabla ya kutia saini makubaliano huko Khartoum Agosti 5, 2018. Kenya Presidential Press Service/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari Michael Makuei ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa mazungumzo yanayoendelea kwa sasa yanakwenda vizuri.

Bw. Michael Makuei amesema, pande hasimu nchini humo zimefikia mwafaka kuhusu mswada wa mkataba wa mwisho wa amani, ambao unatarajiwa kusainiwa Agosti 27, huko Khartoum.

Amesema mazungumzo ya sasa yanahusu masuala ambayo hayajatatuliwa ya kugawana madaraka na mipango ya usalama.

Naye Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom  ametaka pande zote kushughlulikia kwa kikamilifu suala la usalama katika mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.