Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SIASA-USALAMA

Makundi hasimu yatia saini mkataba wa kugawana madaraka Sudan Kusini

Serikali na waasi nchini Sudan Kusini wametia saini mkataba wa kugawana madaraka, ili kumaliza vita vya karibu miaka minne ambavyo vimekuwa vikiendelea katika taifa hilo changa duniani.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto ) na kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar huko Khartoum Agosti 5, 2018.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto ) na kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar huko Khartoum Agosti 5, 2018. © ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo umetiwa saini jijini Khartoum nchini Sudan baada ya pande mbili kukubaliana, baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Kwa mujibu wa makubalino hayo, kiongozi wa waasi Riek Machar atarejea kama Makamu wa kwanza wa rais, katika serikali ya umoja wa kitaifa itakayoongozwa na rais Salva Kiir.

Aidha, imekubaliwa kuwa kutakuwa na mawaziri 35. Rais Kiir atakuwa na mawaziri 20 huku Machar akiwa na tisa huku wapinzani wengine wakigawana nafasi sita zinazosalia.

Pamoja na hilo, kutakuwa na wabunge 550. Upande wa rais Kiir umepewa wabunge 332 huku kundi la Machar likipata wabunge 128.

Baada ya mkataba huu kukubaliwa, rais Kiir na Machar sasa wanatarajiwa kutia saini mkataba wa mwisho hivi karibuni nchini Kenya na baada ya miezi mitatu, serikali hiyo ya Umoja wa Kitaifa itaundwa kuongoza nchi hiyo kwa miezi 36 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.