Pata taarifa kuu
TANZANIA-EAC-MSETO-VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Mseto: Serikali yashindwa kutekeleza maamuzi ya mahakama

Gazeti la Mseto lililosimamishwa kwa madia ya "kueneza habari za uongo na kuchochea machafuko ya umma", limeishutumu serikali ya Tanzania kushindwa kutekeleza maamuzi ya mahakama yanayoitaka kuliacha kuendelea na kazi yake ya kuchapisha habari.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Tarehe 21 Juni, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ilitoa agizo la kufutwa kwa hatua ya serikali ya kusimamisha gazeti la kila siku la Mseto, ambalo lilipigwa marufuku kuchapisha habari kwa miaka mitatu. Hatu hiyo ya serikali ya Tanzania ilichukuliwa mnamo Agosti 11, 2016.

Marufuku hiyo ilichukuliwa kufuatia uchapishaji wa taarifa iliyosema kuwa mshirika wa karibu wa rais John Pombe Magufuli alikubali kupokea rushwa kufadhili kampeni za Bw Magufuli kwa uchaguzi wa mwishoni mwa mwaka 2015.

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam, mmiliki wa gazeti la Mseto, Saed Kubenea, pia Mbunge wa upinzani, aliishutumu serikali kwa kuchelewesha kwa "makusudi utekelezaji wa maamuzi ya mahakama."

"Tanzania, kama mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, inatakiwa kuheshimisha uamuzi huu ... kwa hiyo tutarudi Mahakamani kuomba kibali cha dharura kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa mahakama. ", amesema mwanasheria wa Mseto, Wakili Fulgence Massawe.

Tangu John Pombe Magufuli kuingia madarakani mnamo mwaka 2015, magazeti kadhaa yalifungwa. Sheria zinazozuia uhuru wa kujieleza zilipitishwa nchini humo licha ya maandamano ya mashirika ya haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.