rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Kusini Salva Kiir Riek Machar

Imechapishwa • Imehaririwa

Bunge laongeza muda wa miaka mitatu kwa serikali ya Sudan Kusini

media
Salva Kiir (kushoto),hasimu wake Riek Machar (kulia) na katikati rais wa Sudan Omar al-Bashir, Khartoum.. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Bunge la Sudan Kusini limepitisha Alhamisi wiki hii sheria inayoongeza muda wa miaka mitatu kwa serikali ya mpito nchini humo, ikiwa ni pamoja na muda wa kusalia madarakani kwa rais Salva Kiir.


Wadadisi wanasema hatua hiyo inaweza kuhatarisha mchakato wa amani unaoendelea nchini Sudan Kusini.

"Sheria inayorekebisha Ibara ya 5 ya Katiba ya Mpito kwa mwaka 2018 inapitishwa na bunge la taifa," amesema Spika wa Bunge Anthony Lino Makana, baada ya sheria hiyo kupitishwa kwa kauli moja.

Sudan Kusini imekuumbwa na machafuko tangu mwaka 2015, na kusainiwa kwa mkataba wa amani, ni zoezi lililoongozwa na viongozi wa mpito, ikiwa ni pamoja na serikali na bunge.

Chini ya makubaliano haya, muda wa viongozi hao madarakani utamalizika mnamo Agosti 2018. Serikali imetoa hoja kwamba hatua ya kuongeza muda kwa viongozi wa mpito ilikua muhimu ili kuepuka suala la kutokuepo na taasisi.

"Tunaamini kwamba utaratibu huo ni wa kisheria na kwamba serikali inapaswa kuwa na mamlaka mpya mpaka mkataba mpya wa amani utakapotiliwa saini," kiongozi wa upinzani bungeni, Gabriel Roricjur, ameliambia shirika la habari la AFP.