rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Yoweri Museveni

Imechapishwa • Imehaririwa

Serikali ya Uganda kuangalia upya kodi ya mitandao ya kijamii

media
41% ya raia nchini wanatumia mtandao Uganda kufikia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter iliyo maarufu zaidi nchini humo. REUTERS/Dado Ruvic/Illustration

Serikali ya Uganda imetangaza kwamba itaangalia upya tozo ya kodi ya mitandao ya kijamii na huduma ya kutuma pesa kwa simu nchini humo. Wakati huo huo watu kadhaa wameandamana kupinga kodi iliyoidhinishwa ya kutumia mitandao ya kijamii.


Polisi imefaulu kuzima maandamano hayo baada ya kuwatawanya waandamanaji kwa kufyatua gesi ya kutoa machozi na risasi hewani

Waziri wa habari na mawasiliano Uganda Frank Tumwebaze ametetea kuidhinishwa kwa kodi hiyo, akisema kwamba fedha zitakazopatikana zitatumiwa 'kuwekeza katika rasilmali zaidi za kimitandao'.

Kodi hiyo ya shilingi 200 za Uganda ambayo ni sawa na dola za Marekani 0.05 inayotozwa ili mtu aweze kutumia mitandao kama Twitter na Facebook imechangia kuzuka maandamano nchini.

Baadhi ya wabunge wanashinikiza kodi hiyo isitishwe kwa muda. Bunge litnatarajia kujadili hatua inayofuata Alhamisi wiki hii.

Kodi hiyo iliyoidhinishwa mwanzoni mwa mweiz huu inahitaji watumiaji mitandao ya kijamii nchini kulipa shilingi 200 za Uganda ili waweze kutumia mitandao kama Facebook, Twitter na WhatsApp.

Katika barua aliyomuandikia waziri wa fedha mnamo Machi, rais Museveni amesema kodi kwa mitandao ya kijamii inaweza kuongeza kipato cha serikali, na kupunguza mikopo inayochukua serikali na pesa za ufadhili.