rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenya yatia saini mkataba na Uswisi kusaidia kurejeshwa kwa fedha zilizoibwa

media
Serikali za Kenya na Uswisi zimetia saini makubaliano ya nchi mbili ya kureheshwa nchini Kenya kwa fedha zilizoibwa na kufichwa katika benki za Uswisi. twitter.com/StateHouseKenya

Kenya inaendelea na vita dhidi ya ufisadi nje ya mipaka ya nchi hiyo, baada ya kutia saini mkataba na serikali ya Uswisi, ili kusaidia Mabilioni ya fedha za umma, zilizoibwa na kufichwa katika Benki za Uswisi.


Mkataba huo umetiwa saini na kushuhudiwa na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mgeni wake rais wa Uswisi Alain Berset, aliyemtembelea katika Ikulu ya Nairobi.

Rais Kenyatta amesema, anatumaini kuwa mkataba huo utasaidia kurejesha Shilingi za nchi hiyo Bilioni 72 ambazo ziliibiwa na wafanyikazi wa serikali na kufichwa nchini Uswisi, hasa baada ya kutokea kwa kashfa ya Anglo Leasing.

Aidha, ameongeza kuwa fedha hizo zikirejea zitasaidia kuendesha miradi ya serikali ikiwa ni pamoja na elimu ya bure katika shule za msingi na sekondari.

Mbali na Uswisi, fedha nyingine za wizi zinaamiwa zimefichwa katika kisiwa cha Jersey na nchini Uingereza.

Rais Kenyatta amesema, ameamua kupambana na wizi wa fedha na umma na ufisadi, kamwe hautakubaliwa katika serikali yake.

Nchini Kenya, hivi karibuni, kumeshuhudiwa viongozi mbalimbali akiwemo Gavana wa Kaunti ya Busia, akikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ufisadi, huku rais Kenyatta akisifiwa kwa kuonesha utashi wa kisiasa kupambana na ufisadi.

Makataba kama huu pia, hivi karibuni ulisainiwa nchini Nigeria na kuisaidia nchini hiyo kupata Dola Bilioni 1.2, fedha za umma zilizokuwa zimeibiwa na kufichwa nchini Uswisi.