Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-MAUAJI YA KIMBARI-HAKI

Mamea wawili wa zamani nchini Rwanda wakabiliwa na kifungo cha maisha jela

Mahakama kuu jijini Paris nchini Ufaransa, imependekeza kifungo cha maisha jela kwa Mamea wawili wa Rwanda wanaoshukiwa kuhuska na mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Kesi ya Tito Baharira (katika kiti maalum, upande wa kushoto) na Octavien Ngenzi (upande wa kulia) kuilifunguliwa Mei 10 huko Paris.
Kesi ya Tito Baharira (katika kiti maalum, upande wa kushoto) na Octavien Ngenzi (upande wa kulia) kuilifunguliwa Mei 10 huko Paris. BENOIT PEYRUCQ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Octavien Ngenzi na Titho Barahira wanatuhumiwa kuwa vinara wa mauaji katika tarafa ya Kabaronko.

Mawakili watetezi wanasema walikuwa wanatarajia hilo kutoka kwa muendesha mashtaka.

Leo Alhamisi ndio Mawakili wa washukiwa hao wawili watatoa utetezi wao kabla ya kutolewa kwa hukumu hapo kesho Ijumaa.

Wakati huo huo rais wa Rwanda Paul Kagame, amewahimiza raia wa nchi hiyo kudai huduma wanazozitaka kutoka serikali badala ya kuvuka mipaka na kwenda kuzitafuta katika nchi zingine.

Aidha, amewaambia Wanyarwanda wasalie nyumbani na serikali itawapa wanachotaka.

Kagame ameyasema hayo, baada ya kuzindua kijiji cha kisasa katika eneo la Horenzo, Wilayani Muhanga ambapo nyumba mpya zimejengwa na kuunganishwa na umeme pamoja na maji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.