Pata taarifa kuu
UGANDA-HAKI-UCHUMI

Sheria ya kuwatoza kodi watumianji wa mitandao ya kijamii yaendelea kupingwa Uganda

Wanasiasa, viongozi wa dini na wanaharakati nchini Uganda wameunda vuguvugu la kuishinikiza serikali kuacha kuwatoza kodi, watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Mji mkuu wa Uganda Kampala ambapo inasemekana kuwa kunapatikana watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.
Mji mkuu wa Uganda Kampala ambapo inasemekana kuwa kunapatikana watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii. REUTERS/James Akena/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mamilioni ya watu wanaoshi nchini Uganda wamekuwa wakilipa Shilingiza Uganda 200 kila siku ili kuruhisiwa kutumia mitandao hiyo.

Pamoja na shinikizo hizi, wanaharakati wamekwenda katika Mahakama ya kikatiba kupinga sheria hiyo iliyopitishwa na bunge mwezi uliopita, wakisema inakiuka haki za binadamu.

Wanaharakati hao wakiongozwa na Mawakili wanne ambao ni vijana, wanaitaka Mahakama kuamua kuwa sheria hiyo ni kinyume cha Katiba na inakiuka haki za binadamu.

Sheria hiyo ilianza kutekelezwa tarehe 1 mwezi huu ambayo watumiaji wa mitandao hiyo, walianza kulipia Shilingi 200 kwa siku.

Hii imekuja baada ya bunge mwezi uliipita kupitisha sheria na kuwepo kwa utozwaji ushuru kwa wale wanaotumia mitandao hiyo kama Facebook, Twitter,Instagram, Youtube na Skype miongoni mwa mingine.

Serikali ya rais Yoweri Museveni imesema, fedha zitakazopatikana zitasaidia kufadhili maendeleo mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.