rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Rwanda AU OIF

Imechapishwa • Imehaririwa

Umoja wa Afrika waunga mkono Rwanda kuwania kwenye uenyekiti wa Francophonie

media
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo anatarajiwa kupambana na Mkuu wa sasa wa OIF, Michaelle Jean raia wa Canada, anayewania muhula wa pili. AFP PHOTO/ TONY KARUMBA

Viongozi wa Afrika waliokuwa wanakutana nchini Mauritania, wamekubaliana kuiunga mkono Rwanda kuongoza muungano wa nchi za dunia zinazozungumza lugha ya Kifaransa "La Francophonie" (OIF).


Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo, anatarajiwa kupambana na Mkuu wa sasa wa muungano huo Michaelle Jean raia wa Canada, anayewania muhula wa pili.

Hivi karibuni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliunga mkono Rwanda kuwania kwenye nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya nci zinazozungumza Kifaransa "Francophonieā€¯ (OIF). Baada ya rais Paul Kagame wa Rwanda kuzuru Ufaransa Jumatano wiki hii.

Uungwaji huu mkono kwa mgombea wa Rwanda kwenye nafasi hii ni ishara kubwa ambayo Ufaransa imeonyesha kwa nchi ya Rwanda. Emmanuel Macron alisema katika, kwa vitendo anataka kuonyesha nia yake ya kufufua uhusiano kamili na Rwanda.

Rwanda ni mwanachama wa Francophonie. Baadhi walifikia hata kuamini kwamba tulijitoa katika jumuiya hiyo, lakini sivyo. Tulijiunga na jumuiya nyingine, lakini sisi bado ni mwanachama wa Francophoni, alisema rais Paul Kagame wakati wa ziara yake nchi Ufaransa.