rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania John Pombe Magufuli

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 20 wapoteza maisha kwa ajali nchini Tanzania

media
Picha ikionyesha tukio la ajali lilitokea leo Mkoani Mbeya. Mwananchi

Watu 20 wamepoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari manne Mkoani Mbeya, Kusini magharibi mwa Tanzania.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mussa Athuman Taibu amezungumza na RFI Kiswahili na kuelezea kuhusu tukio hilo.

"Dereva wa lori alikuwa anatoka Mbeya Mjini kwenda Tunduma na alishindwa kulimuda gari akiwa katika mteremko wa Iwambi-Mbalizi na kuyagonga magari mengine matatu ambayo yalitumbukia korongoni"

Kamanda huyo amesema majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kwamba taratibu za utambuzi wa marehemu zinaendelea kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu na mamlaka nyingine.

Matokeo ya ajali za barabarani yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini Tanzania na kugharimu maisha ya watu na mali zao