rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania John Pombe Magufuli

Imechapishwa • Imehaririwa

Tanzania: Rais Magufuli amuondoa kazini waziri wake wa mambo ya ndani

media
Tanzania's president John Pombe Magufuli in Dar es Salaam, October 30, 2015. REUTERS/Sadi Said

Rais wa Tanzania, Dr. John Magufuli amemteua Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi kuchukua nafasi ya Dr. Mwigulu Nchemba.


Haijaelezwa sababu ya kuachwa kwa Mwigulu Nchemba lakini kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Rais ana mamlaka ya ama kuteua au kuwafuta kazi viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo mawaziri.

Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi alipokuwa akizungumza jioni hii kutoka Ikulu ya Magogoni.

Kangi Lugola ni Mbunge anayewakilisha Jimbo la Uchaguzi la Mwibara lililopo wilayani Serengeti , Mkoani Mara, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Mussa Sima, mbunge wa Singida Mjini ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mazingira na Muungano, akichukua nafasi ya Lugola.

Wizara ya Kilimo pia imeongezewa  naibu waziri ambapo Omari Mgumba ameteuliwa kushika wadhifa huo.

Aidha,Rais Magufuli amewateua makamishna wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC na watendaji mbalimbali wa wizara na idara za serikali.