rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Ajali

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 15 wafariki dunia kwa mkasa wa moto Nairobi, Kenya

media
Mkasa wa moto wazuka katika soko la Gikomba, lililokumbwa na mashambulizi mnamo mwaka 2014. REUTERS/Noor Khamis

Watu wasiopungua 15 wamefariki dunia na wengine 70 wamejeruhiwa kwa mkasa wa moto uliozuka katika soko la mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Moto huo ulisambaa kwenye majengo kadhaa na katika eneo jirani.


Mkasa huo ulitokea katika soko la Gikomba, na kitengo cha magari ya wagonjwa cha St John kimerusha picha kwenye ukurasa wake wa Twitter zikionyesha moto huo na vitu vilivyoharibiwa.

Hata hivyo moto huo umedhibitiwa baada ya saa moja na nusu. Chanzo cha moto huo hakijabainika bado.

Ajali za moto nchini Kenya zimekuwa zikitokea mara kwa mara kutokana na miundombinu mibaya ya nyumba za mabanda sambamba na mifumo mibovu ya barabara.

Mapema mwezi Sepemba takribani wanafunzi saba walifariki dunia huku wengine kumi wakijeruhiwa kufuatia moto uliozuka saa nane za usiku katika bweni la shule ya wasichana Moi mjini Nairobi.

Mnamo mwezi Aprili mwaka huu watoto wawili walifariki baada ya kuzuka moto katika nyumba yao wanayoishi majira ya usiku.

Ajali hiyo ya moto ilitokea huko Mukuru, nje kidogo ya mji wa Nairobi ambapo taarifa zilisema kuwa watoto waliofariki ni wakiume wenye miaka miwili huku mwengine wa miaka mitatu wa kike akipokea matibabu hospitalini..

Mwezi Januari mwaka 2017 watu kadhaa walijeruhiwa kwa ajali ya moto uliozuka huko Mukuru.

Mikasa kama hii imekua ikitokea katika nchi mbalimbali na tayari imeuawatu wengi, ikiwa barani Afrika, Ulaya na Amerika.