rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uingereza Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi ya Kenya yahusishwa na kifo cha raia wa Uingereza

media
Maofisa wa polisi wa Kenya wakiwa mbele ya Mahakama Kuu, huku mvua ikinyesha, Nairobi, Kenya, Novemba 14, 2017. AP

Mahakama ya Mombasa imeipata na hatia polisi ya Kenya kwa kuhusika na kifo cha Alexander Monson, raia wa Uingereza aliyeshutumiwa kutumia madawa ya kulevya na ambaye alikutwa alikufa gerezani mwezi Mei 2012 katika mji wa Diani kusini mwa Kenya.


Kwa upande wa familia yake, wamesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 alipigwa hadi kufa, wakati ambapo polisi imedai kuwa alikufa kwa kwa kutumia kiwango kikubwa cha madawa ya kulevya aina ya Cannabis, hoja ambayo imefutiliwa mbali na mahakama.

"Kifo chake hakikuwa cha kawaida na hakikusababishwa na madawa ya kulevya, maisha yake yalifupishwa na polisi," amesema Jaji Richard Odenyo, ambaye amebaini kwamba afisa wanne wa polisi wanapaswa kushtakiwa kwa mauaji. ya Monson.

Mwendesha Mashtaka Mkuu Noordin Haji ameamuru kukamatwa kwa afisaa wanne wa polisi, ambao walitafautiana walipokua wakitoa ushuhuda mahakamani.