rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Kusini Salva Kiir Riek Machar

Imechapishwa • Imehaririwa

Makundi hasimu yatia saini mkataba wa amani Sudan Kusini

media
Kiongozi wa waasi Riek Machar (kushoto) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kulia) wakati wa mazungumzo huko Khartoum na Rais wa Uganda Museveni na Rais wa Sudan al-Bashir (kati) tarehe 25 Juni. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Makundi hasimu nchini Sudan Kusini yametia saini leo Jumatano mjini Khartoum, nchini Sudan, mktaba wa amani, huku wakikubaliana kusitisha mapigano ndani ya saa 72 zihazo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Al-Dirdiri Mohamed Ahmed amesema.


Mkataba huu pia unaeleza kuachiliwa huru kwa wafungwa, utoaji wa misaada ya kibinadamu na kuundwa kwa serikali ya mpito ndani ya miezi minne.

Hata hivyo msemaji wa waasi amekataa baadhi ya vipengele vya mkataba huo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar na viongozi wengine wa upinzani wamesaini mkataba huo wakati wa sherehe rasmi iliyofanyika hadharani mjini Khartoum.

Msemaji wa Riek Machar, hata hivyo, amesema waasi wamekataa kutumwa kwa waangalizi wa Umoja wa Afrika watakaofuatilia uheshimishwaji wa kusitishwa kwa mapigano, pamoja na mipango ya kutenga miji mitatu ambako idadra mbalimbali za serikali zitahamishwa.