rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania John Pombe Magufuli

Imechapishwa • Imehaririwa

Bakhressa kuzindua kampuni mpya ya mawasiliano, Tanzania

media
Said Salim Bakhressa akiwa na Rais wa Tanzania Dr.John Magufuli Haki Pension blog

Mfanyabiashara mashuhuri nchini Tanzania, Said Salim Bakhressa anatarajia kuzindua kampuni mpya ya mawasiliano itakajolukikana kwa jina la Azam Telecommunication (T) Limited.


Bakhressa, anamiliki mtandao wa makampuni ya Azam yanayojumuisha viwanda wa matunda, vyakula, vinywaji na vyombo vya habari. Kampuni hizi umesambaa katika mataifa mbalimbali yaliyopo mashariki na Kusini mwa Afrika, kama Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Msumbiji, Zambia, Sudan Kusini na Burundi.

Ripoti zilizochapishwa na vyombo vya habari nchini Tanzania leo, zinasema kampuni ya Azam Telecommunication Limited itaingia sokoni hivi karibuni na kuongeza ushindani kwenye mauzo ya vifurushi vya data, muda wa maongezi na huduma nyingine.

Msemaji wa Kampuni hiyo, Hussein Sufian amenukuliwa na gazeti la Mwananchi, akiarifu kuwa utaratibu ukikamilika watanzania wataanza kufurahia huduma za kampuni hiyo zitakazokuwa na bei ya chini zaidi.Aidha amepasha kuwa mipango inafanyika kuhakikisha kampuni hiyo inakuwa na mtandao nchi nzima.

Mwandishi wa RFI Kiswahili, Emmanuel Makundi anasema ujiuo wa kampuni hiyo utakuwa na manufaa kwa kutoa ajira kwa wananchi.

Uwekezaji huu mpya unakuja wakati serikali ya Tanzania ikinuia kuimarisha uchumi wa taifa hilo kupitia sera ya viwanda kufikia 2025.