rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uhuru Kenyatta Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais Kenyatta atangaza ukaguzi wa maisha ya wafanyakazi wa serikali

media
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta REUTERS/Thomas Mukoya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa serikali yake itafanya zoezi la ukaguzi wa aina ya maisha wanayoishi wafanyakazi wa umma.


Rais Kenyatta amesema wafanyakazi wote wa umma akiwemo yeye mwenyewe na Naibu wake William Ruto watatakiwa kutoa maelezo ya mali wanazomiliki na wale watakaobainika kuiba fedha za umma watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

“Tunataka kufahamu hiyo mali uliyonayo, uliipata vipi, haki ya Mungu, lazima wizi wa mali ya wananchi wa Kenya uishe,”alisema rais Kenyatta akiwa mjini Mombasa.

Kauli ya rais Kenyatta imekuja wakati huu nchi hiyo ikishuhudia kampeni kubwa ya kupambana na vitendo vya rushwa ambapo hivi karibuni maofisa kadhaa wa Serikali walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ubadhilifu wa mali za uma na matumizi mabaya ya ofisi.

Maafisa wa serikali na watu wengine zaidi ya 40 wameshtakiwa kwa wizi wa Mamilioni ya Dola zilizokuwa zimetengewa Shirika la huduma kwa vijana NYS.