rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Kusini Salva Kiir Riek Machar

Imechapishwa • Imehaririwa

Riek Machar akubali kukutana na Salva Kiir

media
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto) na kiongozi wa waasi Riek Machar (kulia). EUTERS/Goran Tomasevic (

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar amekubali, kukutana na rais Salva Kiir jijini Addis Ababa wiki ijayo. Machar amealikwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, kukutana na mpinzani wake na kuona namna ya kurejesha amani katika nchi yao.


Mazungumzo mapya yamepangwa kufanyika tarehe 20 mwezi huu, chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya chi za Afrika Mashariki IGAD ambazo zitaendelea kuwapatanisha viongozi hao.

Hayo yanajiri wakati ambapo Marekani imetaka Serikali ya Kenya kuchunguza mali zinazomilikiwa na familia za wasomi kutoka Sudan Kusini, zikiwemo mali za aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir, mali ambazo Marekani inasema viongozi hao wamewekeza nchini Kenya.

Marekani inasema inao ushahidi wa kutosha kuonesha namna familia na viongozi wa Sudan Kusini wamekuwa wakiwekeza nchini Kenya kwa kutumia fedha za uma huku wengi wakiwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo.