rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Yoweri Museveni

Imechapishwa • Imehaririwa

Polisi Uganda: Hali ya usalama imedhibitiwa

media
Polisi ya uganda imewahakikishia raia kuwa hali ya usalama imedhibitiwa, baada ya kushuhudiwa hivi karibuni visa vya mauaji. Reuters/James Akena

Jeshi la Polisi nchini Uganda limewatoa hofu ya usalama wananchi wa taifa hilo baada ya hivi karibuni kushuhudiwa kwa matukio ya watu kuuawa na kutekwa na watu wasiojulikana, matukio ambayo yamesababisha sintofahamu nchini humo.


Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Uganda, Martin Ochola amesema anashangazwa na matamshi ya baadhi ya wanasiasa wanaodai kuwa hali ya usalama nchini humo imezorota.

Matamshi ya IGP Martin Okoth Ochola yanakuja ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu watu wasiofahamika wamuue mbunge mmoja jijini Kampala hatua iliyomfanya rais Yoweri Museveni kutangaza marufuku ya kuvaa makoti makubwa kwa waendesha bodaboda.

Visa hivi vya mauaji vimewatia wasiwasi raia wa nchi hiyo, huku wakiomba usalama uimarishwe vilivyo na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali wanaohusika na mauaji hayo.