Pata taarifa kuu
UGANDA-MAUAJI

Raisi Museven aapa kuwashughulikia wauaji Uganda

Raisi wa Uganda Yoweri Kaguta Museven amesema yeyote anayeua raia wa Uganda atashughulikiwa bila kusita,akikosoa uhasama wa kisiasa kusababisha chuki na mauaji nchini humo.

Raisi wa Uganda Yoweri Museven
Raisi wa Uganda Yoweri Museven GAEL GRILHOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akiwa katika sherehe za mashujaa wilayani Kakumiro jumamosi Raisi Museven ameapa kulipa kisasi kwa yeyote anayemwaga damu ya raia wa Uganda.

Kauli hiyo inakuja muda mfupi baada ya mauaji ya mbunge wa manispaa ya Arua kanali mstaafu Ibrahim Abiriga na ndugu yake Saidi Butele waliokuwa katika klabu ya usiku jirani na kawanda,wilayani wakiso.
Kanali mstaafu Ibrahim Abiriga,mbunge wa chama tawala chake raisi Museven NRM alikuwa akiunga mkono mabadiliko ya katiba yaliyopendekezwa mwaka jana Decemba yakilenga kufuta kipengele cha ukomo wa umri wa kuwania uraisi nchini Uganda.

Abiriga,ambaye ameuawa akiwa na umri wa miaka 62,aliunga mkono mabadiliko hayo ambayo yanatajwa kumpa nafasi raisi Museven ambaye amekuwa madarakani tangu 1986 kuendelea kutawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.