rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Ajali

Imechapishwa • Imehaririwa

Zoezi la kutafuta ndege iliyotoweka laendelea Kenya

media
Ndege hiyo iliokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta , iliondoka Kitale, muda mfupi kabla ya saa kumi jioni ikiwa na abiria wanane na wafanyikazi wawili na ilitarajiwa kuwasili Nairobi saa moja baadaye. SIMON MAINA / AFP

Baadhi ya maafisa wa utafutaji na uokoaji walikuwa wakitarajiwa kusafirishwa kwa ndege kutoka katika uwanja wa Njambini ili kupelekwa katika eneo la utafutaji mwendo wa saa moja alfajiri.


Kulingana na taarifa ya mkuu wa mamlaka ya usafiri wa angani nchini Kenya zoezi la utafutaji wa ndege hiyo ambao ulikuwa ukiendelea ulisimamishwa kwa muda na ulitarajiwa kuendelea Jumatano hii alfajiri.

Ndege hiyo iliokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta , iliondoka Kitale, muda mfupi kabla ya saa kumi jioni ikiwa na abiria wanane na wafanyikazi wawili na ilitarajiwa kuwasili Nairobi saa moja baadaye.

Ndege hiyo nyepesi ya kubeba abiria aina ya Cesna C208 ilio na nambari ya usajili ya Y-CAC kutoka Kitale Magharibi mwa Kenya , ilipoteza mawasiliano na mnara wa kudhibiti ndege muda wa saa kumi na moja jioni siku ya Jumanne katika eneo la Aberdares, yapata kilomita 60 kabla ya kufika eneo ililokuwa ikielekea.

Ndege hiyo inasimamiwa na kampuni ya ndege ya East Africa Safari Air Express,

Taarifa kutoka kwa kampuni hiyo zinasema kuwa ndege hiyo ilitoweka lakini juhudi za pamoja zinazoshirikisha mashirika ya wanyama pori KWAS na kitengo cha kuchunguza ajali za ndege zimekuwa zikiendelea kuisaka ndege hiyo.

Ishara za simu kutoka kampuni ya ndege ya FlySax ambayo ilitoweka siku ya Jumanne jioni zimepatikana katika eneo la Aberdares katika kaunti ya Nyandarua nchini Kenya, kwa mujibu wa Naibu mkurugenzi wa shirika la wanyama pori nchini Kenya anayesimamia maeneo ya milima, Simon Gitau.