rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania John Pombe Magufuli

Imechapishwa • Imehaririwa

Mapacha walioungana Tanzania, wafariki dunia

media
Maria na Consolata, pacha waliofariki dunia jana Mkoani Iringa Mwananchi

Watanzania wanaomboleza vifo vya pacha wa kipekee waliougana nchini humo Maria na Consolata Mwakikuti, waliofariki dunia jana katika hospitali ya rufaa ya mkoa waIringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania.


Mapacha hao waliokuwa wanasomea Ualimu katika VChuo kikuu cha kikatoliki cha Ruaha kilichopo Mkoani Iringa, wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo ya moyo, na kuanzia mwaka 2017 wamekuwa wakipata matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter alitoa taarifa ya vifo vya mabinti hao waliokuwa wakipendwa na mamilioni ya watanzania.

Maafisa wa juu wa nchi hiyo wakiongozwa na rais John Magufuli wamesema wamesikitishwa na kifo cha mapacha hao wa kipekee.

"Nimesikitishwa na vifo vya Maria na Consolata ambao walikuwa na ndoto ya kulitumikia taifa,"alisema Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Aidha, Vifo vya mabinti hawa vimepelekea simanzi miongoni mwa watanzania ambao wamemiminika kwenye mitandao ya kijamii kuwalilia Maria na Consolata Mwakikuti, wanasiasa, wasanii wakiwa miongoni mwao.

Mwaka jana katika mahojiano waliyofanya na vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania, walieleza ndoto yao ni kuwa walimu, pindi watakapomaliza masomo ya juu.

Gazeti la kila siku la Mwananchi limemnukuu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, akisema mapacha hao walipishana dakika kumi.

Maria na Consolata wamelelewa na shirika la masista wa kanisa Katoliki la Maria Consolata, baada ya wazazi wao kupoteza maisha wakiwa wadogo

Ripoti zaidi zitakujia, endelea kufuatilia mtandao wetu