Pata taarifa kuu
UGANDA-MITANDAO YA KIJAMII-KODI

Kodi kwa mitandao ya kijamii Uganda itakandamiza uandishi wa habari

Shirika la kimataifa la waandishi wa habari wasio na mipaka limelaani kikwazo cha kukusanya taarifa na kuropoti nchini Uganda kufuatia sheria mpya inayotoza kodi ya kila siku kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Raisi wa Uganda Yoweri Museven
Raisi wa Uganda Yoweri Museven REUTERS/Hannah McKay
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia juali mosi na kuendelea watumiaji wa mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter, Skype na nyinginezo kama hizo watapaswa kulipia kodi ya kila siku ya kiasi cha dola 5 za Marekani ili kuweza kuendelea kutumia huduma hizo.

Bunge lilipitisha sheria hiyo mnamo May 30 kutekeleza kile raisi Yoweri Museven alitangaza ni kudhibiti habari za kughushi mitandaoni.

Miongoni mwa walioguswa na sheria hiyo ni wamiliki wa blogu na waandishi wa habari ambao bado wanatumia mitandao ya kijamii kujieleza kwa uhuru zaidi kuliko katika vyombo vingine vya habari nchini humo.

Rosebell Kagumire moja kati ya wamiliki wa blogu maarufu yenye ushawishi nchini Uganda ameliambia Shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka kuwa katika mazingira ya kunyimwa uhuru wa vyombo vya habari mitandao ya kijamii imetumika kama jukwaa la mijadala ambayo imekuwa ikikosoa serikali ya raisi Museven.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.