rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Yoweri Museveni

Imechapishwa • Imehaririwa

Raia wanaotumia mitandao ya kijamii kutozwa kodi Uganda

media
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ambaye serikali yake imechukua hatua ya kutoza kodi mitandao ya kijamii nchini humo.. REUTERS/James Akena

Wananchi wa Uganda wameendelea kuilalamikia serikali ya nchi yao kuhusu hatua mpya iliopitishwa hivi majuzi na bunge kupitisha muswada tata wa kodi kwa watumiaji wa mitandano ya kijamii na huduma za miamala ya kifedha kwa njia ya simu.


Kwa siku, kila mtu anayetumia mitandao kama vile facebook, WhatsApp Viber na Twitter anatakiwa kulipa shillingi mia mbili za nchi hiyo kiwango ambacho wananchi wanasema ni kikubwa mno ukilinganisha na kipato chao kwa siku.

Rais Museveni alisisitiza kuhusu muswada huo akidai kuwa mabadiliko ni muhimu na kwamba mitandao ya kijamii imekuwa ya kwanza kusambaza umbea na habari zisizokuwa na uhakika.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya RFI, Monica Amoding, ambaye ni mmoja wa wabunge wa chama tawala cha NRM amesema anapinga kupitishwa kwa muswada huu.

Sheria hiyo inatakiwa kuanza kutekelezwa ifikapo Julay 1. lakini kabla ya hapo tayari kumeanza kuwa na mashaka juu ya utekelezwaji wake.