rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uhuru Kenyatta Raila Odinga Uchaguzi Kenya 2017

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenyatta na Odinga waomba radhi kwa uchaguzi wa Kenya

media
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) na kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga. TONY KARUMBA, SIMON MAINA / AFP

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wameomba radhi Alhamisi wiki hii kwa kauli zao zilizosababisa vifo wakati wa uchaguzi tata mnamo mwaka 2017. Kitendo hiki ni ishara inayounga mkono ahadi zao za kuboresha maridhiano nchini.


Baada ya kupeana mkono, mnamo mwezi Mach, kitendo ambacho kilishangaza wengi, na kuashiria kusitishwa kwa mvutano kati ya wawili hawa, Alhamisi wiki hii Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wamejikuta wako pamoja, kila mmoja akimsabahi mwingine kwa furaha kubwa wakati wa "ibada ya kitaifa" iliyofanyika mjini Nairobi, tukio la kila mwaka ambapo viongozi wa kisiasa wanafanya maombi kwa taifa hilo.

Katika hali ya kuimarisha wigo wa utekelezaji wa ahadi zao, wawili hawa, ambao kila mmoja amekua akimwita mwengine "ndugu yangu", wameandamana leo Alhamisi na Makamu wa rais William Ruto na mgombea mwenza wa Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, ambao pia wameomba radhi na kukiri kumaliza uhasama kati yao, ikiwa ni tukio la kwanza tangu uchaguzi.

"Tulifanya kampeni ambapo kila mmoja alimkashifu mwengine, tulisema mambo mabaya kila mmoja kwa mwegine, na leo ninaomba radhi," amesema rais Uhuru Kenyatta, aliyechaguliwa tena kwa muhula wake wa mwisho mnamo mwaka 2017, kabla ya watatu wengine kupewa nafasi kufanya hivyo.

"Hakuna Mkenya atarudi tena kupoteza maisha kwa sababu ya uchaguzi," Odinga ameongeza, akimaanisha miezi ya vurugu ambayo ilifuatia uchaguzi wa mwaka 2017 ambapo watu zaidi ya 100 waliuawa, wengi wao na polisi.