rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

CCM John Pombe Magufuli Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

Dr. Bashiru Ali ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania

media
Katibu Mkuu mpya wa Chama tawala nchini Tanzania, Dr. Bashiru Ali screenshot/Ikulu

Chama tawala nchini Tanzania, CCM kimemteua Dr. Bashiru Ali kuwa katibu mkuu wake mpya akichukua nafasi ya Abdulrahman Kinana.

 


Kinana alitangaza kung'atuka katika nafasi yake Mei 28 mwaka huu baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kwa miaka saba.

Uteuzi wa Ali umefanywa na mwenyekiti wa chama hicho na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Magufuli na kuthibitishwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho katika kikao chake kilichoketi jana, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, Dr. Bashiru Ali alikuwa mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ambaye aliongoza mchakato wa kuhakiki mali za CCM.

Kabla ya kuteuliwa kushika nafsi hiyo, Dr. Bashiru Ali akuwa mhadhiri mwandamizi katika idara ya sayansi ya siasa, Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) na alikuwa akiongoza kurugenzi ya mijadala na makongamano.

“Tumekupa dhamana hii katika kipindi kigumu,”imesema taarifa ya chama hicho.

Makamu Mkuu mstaafu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandara amenukuliwa na gazeti la kila siku la Mwananchi akisema hana shaka na Dr. Bashiru kutokana na uzeofu wake katika mijadala na kuwa miongoni mwa wasomi wa ngazi ya juu.

Hata hivyo, Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Mtama,kusini mwa Tanzania, Nape Nnauye alitumia ukursa wake wa Twitter kuandika kuhusu Kinana kuwa alikuwa mwalimu aliyebadili mtazamo wake kuhusu siasa na utumishi wa umma.