rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya

Imechapishwa • Imehaririwa

Washukiwa 54 wa ufisadi kufikishwa mahakamani Kenya

media
Gari lililobeba watuhumiwa kwenye makao makuu ya mamlaka ya uchunguzi wa makosa ya jinai, Nairobi, Mei 28, 2018. REUTERS/Baz Ratner

Washukiwa 54 wa ufisadi wanaoshtumiwa kuiba Dola za Marekani, Milioni 80 zilizotengewa Shirika la huduma kwa vijana NYS, wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani.


Miongoni mwa washukiwa hao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana, Lilian Omolllo na Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai.

Rais Uhuru Kenyatta amesema, serikali yake haitaruhusu watu waiso na maadili.

Kiongozi wa Mastaka nchini humo Noordin Mohammed Haji amesema kuna ushahidi wa kutosha kuwapata na hatia washukiwa hao.

Bw Haji amesema kuwa washukiwa 54 wanapaswa kufikishwa mahakamani Jumanne wiki hii kuhusiana na sakata ya NYS.

Haji amesema kuwa ofisi yake itaendelea na uchunguzi hadi pale wote waliohusika wamehukumiwa kisheria.

Kwa mujiu wa Haji kupambana na ufisadi kutachukua muda.

Kaunti za benki za washukiwa zimezuiliwa na serikali. Bw Haji amewataka wale wote walio na ushahidi kuhusu sakata zilizoripotiwa kufika kwenye ofisi yake. Tayari serikali imepania kuanzisha operesheni ya kuchukua mali zao, mara baada tu ya kupatikana na hatia.