rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 48 wapoteza maisha katika ajali nchini Uganda

media
Raisi wa Uganda Yoweri Museven GAEL GRILHOT / AFP

Jumla ya watu 48 wamepoteza maisha kaskazini mwa Uganda baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na trekta,shirika la msalaba mwekundu limearifu jumamosi baada ya polisi awali kutoa idadi ya watu 22.


Msemaji wa polisi nchini Uganda Emilian Kayima alifahamisha kuwa majeruhi 14 wa ajali hiyo iliyohusisha magari matatu usiku wa kuamkia jumamosi walikimbizwa hospitali wakati madereva wote watatu wakiwa ni miongoni mwa waliofariki.

Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa jumla ya vifo ni 48 wakiwemo watoto 16.

Hata hivyo jeshi la polisi nchini humo limeendelea kutaja idadi ya vifo 22 wakiwemo watoto 3 huku Vyombo vya habari nchini humo vikiripoti jumla ya watu 30 kupoteza maisha.

Mnamo mwaka 2015 raisi wa taifa hilo Yoweri Museven aliwafuta kibarua takribani watumishi 900 wanaohusika katika ujenzi wa barabara nchini humo kwa kufanya kazi hiyo chini ya kiwango na kuchangia ongezeko la ajali nchini humo.