Pata taarifa kuu
BURUNDI-ZAMBIA-COMESA-UCHUMI-USALAMA

Mkutano wa COMESA kufanyika Lusaka, Zambia Julai 2018

Licha ya nchi ya Burundi kupata pigo la kisiasa na kidiplomasia kwa kukataliwa kuandaa mkutano wa nchi za jumuiya ya soko la pamoja COMESA kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo, Serikali ya Bujumbura yenyewe bado inaendelea na maandilizi ya mkutano huo.

Polisi na askari wakipiga doria katika moja ya mita ya Bujumbura, huku serikali ya Bujumbura ikiendelea na maandilizi ya mkutano wa COMESA.
Polisi na askari wakipiga doria katika moja ya mita ya Bujumbura, huku serikali ya Bujumbura ikiendelea na maandilizi ya mkutano wa COMESA. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama
Matangazo ya kibiashara

Maandalizi ya Serikali ya Burundi yanafanyika licha ya siku chache zilizopita katibu mkuu wa Jumuiya ya COMESA kuiarifu Serikali kuahirishwa kwa mara nyingine kwa mkutano huo uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi ujao.

Licha ya COMESA kutoeleza sababu rasmi za kuahirisha kufanya mkutano huo, wadadisi wa masuala ya kikanda wanaona uamuzi huo umetokana na hali tete ya kisiasa nchini Burundi pamoja na kufanyika kwa kura tata ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyozungumza na idhaa yetu vimedai kuwa Serikali ya Bujumbura haijapokea barua yoyote kutoka COMESA kuhusu kuahirishwa kwa mkutano huo hatua inayoufanya utawala uendelee na usajili wa wageni na kuimarisha usalama.

Mpaka sasa kuna taarifa kuwa ni nchi 2 tu SyeChelles na Zambia kati ya nchi wanachama 18 ambazo zilithibitisha viongozi wake kuhudhuria mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.