rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Burundi Pierre Nkurunziza Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 26 wauawa Burundi baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana

media
Eneo lililoshambuliwa Kaskazini Magharibi mwa Burundi AFP PHOTO / Carl DE SOUZA

Watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami kwa silaha wameuwa watu 26 Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Burundi.


Ripoti zinasema,mauaji haya yalitokea siku ya Ijumaa usiku, huku wenyeji wakivamiwa kwa kupigwa risasi na kuchomwa visu.

Afisa wa serikali ambaye hakutaka kutajwa, ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa amehesabu miili 23.

Waliouawa ni pamoja na wanaume, wanwake na watoto na huenda idadi ikaongezeka.

Watu wengine zaidi ya 10 wameripotiwa kujeruhiwa katika uvamizi huo huku polisi walisema kuwa wanafanya uchunguzi.

Haijafahamika watu walioptekeleza uvamizi huo ni akina nani, lakini wakaazi wa kijiji hicho katika mkoa wa Citiboke wanashuku kuwa huenda wamevuka mpaka kutka nchi jirani ya DRC.

Mauaji haya yamekuja, kuelekea zoezi la kura ya maoni tarehe 17 kuibadilisha Katiba ya nchi hiyo, kumwezesha rais Pierre Nkurunziza kuendelea kukaaa madarakani hadi mwaka 2034.