Pata taarifa kuu
KENYA-MAJANGA-ASILI

Kenya yajaribu kuepukana na madhara yanayosababishwa na mvua zinazonyesha

Serikali ya Kenya itaharibu mabwawa mengine mawili ya maji katika eneo la Solai, baada ya maji kuvunja kingo za bwawa moja na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Bwawa la Patel likivunja kingo zake katika mji wa Solai na kusababisha mtiririko wa maji ya matope, yaliyoharibu nyumba nyingi na watu wengi kupoteza maisha.
Bwawa la Patel likivunja kingo zake katika mji wa Solai na kusababisha mtiririko wa maji ya matope, yaliyoharibu nyumba nyingi na watu wengi kupoteza maisha. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kuharibu mabwawa hao mawili yaliyofahamika kama Marigu na Milmet linaongozwa na jeshi la nchi hiyo, ili kuepuka janga lingine kama lile lililotokea siku ya Jumatano usiku.

Gavana wa Kaunti ya Nakuru Lee Kinyajui amesema hatua hii imechukuliwa baada ya watalaam kuthamini mabwawa hayo na kusema kuwa sio salama kwa wakaazi wa eneo hilo.

Kabla ya hatua hii, kulikuwa na wasiwasi kuwa maji ya mabwawa hao mengine huenda yangevunja kingo zake na kusababisha mauaji na uabarifu mkubwa kama ilivyoshuhudia.

Wakati hayo yakijiri, watalaam wa ukoaji wameendelea na zoezi la kutafuta miili zaidi baada ya kuripotiwa kuwa kuna watu zaidi ya 40 bado hawajapatikana, hali ambayo inazua hofu kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Mbali na mauaji haya, mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha nchini humo imeleta mafuriko makubwa na kusababisha zaidi ya watu 170 kupoteza maisha, na maelfu kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.