rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Rwanda

Imechapishwa • Imehaririwa

Rwanda yachukua uamuzi wa kuwahamisha raia wanaoishi katika maeneo hatari

media
Mji wa Kigali, Rwanda. Getty/Peter Stuckings

Serikali ya Rwanda imeanza zoezi la kuwahamisha kwa nguvu baadhi ya wakazi wa mitaa ya Kigali wanaoishi katika maeneo hatari na kuwapa hifadhi kwenye makanisa yaliyonyang’anywa vibali vya kuendesha shughuli za kidini mapema mwaka huu.


Wakazi wapatao 100 waliokuwa wanaishi katika maeneo hatari ya jiji la Kigali wamejikuta wanahamishwa kwa nguvu na zoezi hilo linaendelea.
Wengi wao wamesikika wakifurahia kampeni hiyo huku wengine wakiikosoa serikali.

“Mie nina familia ya watu watano. Jioni hii Kifusi cha Udongo kimeangukia nyumba yangu. Kusema kweli hatuwezi kupinga maamuzi ya serikali kwani chochote itakachotufanyia tutakitii, “ amesem amkaazi mmoja wa Kigali.

“Kitu ambacho kimekiukwa hapa, baadhi ya watu wamelala njaa bila  hata maji ya kunywa. Eneo hili ambalo halina hata maji, tutegemee kutokea miripuko ya maradhi. eneo hili ni la kanisa lililofungwa liitwalo SHILO. Hebu fikiria hapa walipafunga kutokana na kile ambacho serikali iliona hapafai lakini leo sisi eti panatufaa, hii ni kweli?, “ amesema mkaazi mwengine.

Viongozi mbalimbali wa serikali za mitaa, wameishauri wizara ya majanga kuchukua tahadhari mapema kabla magonjwa ya mlipuko hayajatokea mahali walipohifadhiwa kwa muda. Bi:

“Tunaomba serikali itusaidie na ifanye hima watu hawa waondoke mahali hapa, kwa vile serikali iliona kanisa hili ina maana hapakupaswa kutumiwa na mtu yeyote kutokana na kutokidhi vigezo, wakati wowote mvua itanyesha na mahali hapa hakuna hata choo, mimi naona yafaa wapelekwe mahali pengine. Kaya 19 zilizopo hapa ina jumla ya watoto 50 na wengi wao wana miaka 5,” amesema Mukaruvugiro Winfried, kiongozi anayehusika na maswala ya kijamii katika kijiji cha Birima, tarafa ya kimisagara jijini Kigali..

Kwa upande wa Wizara ya majanaga MIDIMAR imesema kuwa kitu cha kwanza wanachofanya ni kuwahamisha watu. Huyu hapa ni.
“Tunachokifanya kwa sasa ni kuwahamisha watu wanaoishi maeneo ambayo si salama na kuwapeleka katika maeneo salama, wasio na uwezo tunawasaidia, “ amesema Alphonse Hishamunda  kiongozi anayepambana na majanga kutoka wizara ya majanga MIDIMAR.

Hadi sasa zaidi ya watu 200 wameshapoteza maisha huku idadi ya watu waliojeruhiwa na vitu vilivyoharibika ikiwa bado haijajulikana.