rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Bwawa lavunja kingo zake na kuua watu wengi Kenya

media
Mafuriko yasababisha madhara makubwa Isinya, kilomita 60 kusini masharuiki mwa Nairobi, Machi 15, 2018. TONY KARUMBA / AFP

Watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha na zaidi ya 40 kujeruhiwa baada ya kuvunjika kwa kingo za bwawa la maji katika eneo la Solai katika Kaunti ya Nakuru, karibu Kilomita 200 Kaskazini mwa jiji kuu Nairobi nchini Kenya.


Janga hilo lilitokeausiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii, wakati wakaazi wa Solai walipokuwa majumbani mwao, wengi wakiwa wamelala wakati waliposombwa na maji.

Watoto ni miongoni mwa watu walipoteza maisha katika janga hilo baya kuwahi kutokea nchini humo, na limetokea wakati huu, nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Awali Gavana wa mkoa wa Nakuru alisema kiwango cha uharibifu kinaendelea kutathminiwa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limetangaza kwenye Twitter kwamba limewaokoa watu 39.

Kupasuka kwa bwawa hili kumesababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha mashariki mwa Afrika kwa miezi miwili sasa.

Mbali na maafa hayo, mamia ya watu wamepoteza makwao na kusalia wakimbizi baada ya tukio hilo, kwa mujibu wa shirika la Msalaba mwekundu

Tangu mwezi Machi, mvua hizo zimeua watu 132 na kusababisha zaidi ya watu 220,000 kuyahama makazi yao katika kaunti 32, serikali ya Kenya imesema.