rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Kusini Riek Machar Salva Kiir

Imechapishwa • Imehaririwa

Sudan Kusini: Wapiganaji wa upinzani wadaiwa kushambulia mji wa Pagak

media
Wapiganaji wa upinzani nchini Sudan Kusini REUTERS/Goran Tomasevic

Serikali ya Sudan Kusini imewashtumu waasi wa upinzani SPLM-IO wanaongozwa na Makamu wa rais wa zamani Riek Machar kwa kushambulia mji wa Pagak na kuvunja makubaliano ya kutoendelea na mapigano katika eneo hilo.


Kanali Dickson Gatluak Msemaji wa jeshi linalalomuunga mkono Makamu wa kwanza wa rais Taban Deng Gai amethibitisha mashambulizi hayo.

Aidha, ameeleza kuwa ilibidi wanajeshi wake kujibu mashambulizi hayo lakini hakueleza iwapo kulikuwa na maafa au majeruhi .

Makabiliano haya yamekuja kuelekea mazungumzo mapya ya amani yaliyopangwa kufanyika kuanzia tarehe 17 mwezi huu jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kati ya waasi na serikali ya Juba.

Wiki hii,  rais wa Uganda  Yoweri Museveni alizuru jijini Juba na kufanya mazungumzo na rais Salva Kiir na viongozi wa chama tawala SPLM kuhusu amani ya nchi hiyo.

Kabla ya kwenda jijini Juba, alikutana na wanasiasa wa upinzani jijini Kampala.

Uganda inasalia mojawapo ya nchi muhimu katika utatuzi wa mzozo wa Sudan Kusini.

Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wanapewa hifadhi nchini Uganda, kwa sababu ya vita vinavyoendelea.