Pata taarifa kuu
BURUNDI-KATIBA-SIASA-USALAMA

Kanisa Katoliki: Huu sio wakati muafaka wa kuifanyia mabadiliko Katiba ya Burundi

Kanisa Katoliki lenye waumini wengi nchini Burundi limeelezea wasiwasi wake kuhusu marekebisho ya Katiba, siku mbili baada ya kampeni za kuifanyia mabadiliko Katiba hiyo kuanza rasmi.

Baraza la Maaskofu wa Kanisa katoliki nchini Burundi.
Baraza la Maaskofu wa Kanisa katoliki nchini Burundi. Esdras Ndikumana / RFI
Matangazo ya kibiashara

Kura ya maoni imepangwa kufanyika Mei 17 na ambayo inatamruhusu Rais Pierre Nkurunziza kubaki mamlakani hadi mwaka 2034.

Ukosefu wa suluhisho katika mgogoro wa kisiasa unaoikumba nchi hii kwa miaka mitatu, hali ya hofu inayoendelea kuwakabili wananchi wa taifa hilo dogo la Afrika ya kati.

Kutokana na hali hiyo Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Burundi limesema kuwa haikuwa wakati mzuri wakuifanyia mabadiliko ya kina katiba ya Burundi.

Pia baraza hilo linabaini kwamba rasimu hii ya marekebisho ya Katiba haikuzingatia kifungu cha 299 cha Katiba ya sasa kwa sababu katiba hiyo haiji kuunganisha Warundi.

"Ibara hii inasema kuwa hakuna utaratibu wa marekebisho ambao utazingatiwa ikiwa utakuja kudhoofisha umoja wa kitaifa, maendeleo ya wananchi wa Burundi na maridhiano," ameeleza Mwenyekiti wa baraza hilo, Askofu Joachin Ntahondereye. Kwa mujibu wa kile tunachokiona, badala ya kuunganisha Warundi, kazi iliyofanyika na rasimu ya Katiba iliyopitishwa na serikali vimekuja kuzidisha vurugu na kukuza chuki baina ya wananchi wa Burundi. Kwa maoni yetu, kama tulivyosema, wakati huo sio muda muafaka wa kuifanyia mabadiliko Katiba ya nchi. Lakini kwa kuwa kwa njia ya kidemokrasia ambayo nchi yetu imechukua, kura ina neno la mwisho kuhusu maswali haya, inabakia tu tuombe kura ya maoni ifanyike kwa amani na kwa uhuru, na kwamba bila shinikizo lolote Warundi watapiga kura kwa uhuru Ndiyo au Hapana. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.