rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Rwanda DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Rwanda yafuta uongozi wa wakimbizi wa kambi ya Kiziba

media
Kambi ya wakimbizi ya Kiziba, Rwanda. DR

Serikali ya Rwanda, imefuta uongozi wa wakimbizi wa kambi ya kiziba magharibi mwa Rwanda , kwa sababu ya vurugu ambazo zimekuwa zikishuhudiwa katika kambi hiyo katika siku za hivi karibuni.


Hatua hii imekuja miezi kadhaa baada ya vurugu zinazoendela kwenye kambi hiyo kutokana na maandamano yaliyofanywa na wakimbizihao mwezi Februari mwaka huu ,wakipinga kupungua kwa msaada wao wa chakula na kutishia kurejea nyumbani.

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wabeba vitu vyao wakipita karibu na ofisi ya UNHCR kwenye kambi ya wakimbizi ya Kiziba, Rwanda, Februari 21, 2018. Jean Bizimana / REUTERS

Kwa upande wa uongozi huo wamesema hawakubaliani na hatua hiyo na kutangaza kua hawataachia uongozi hadi muda wao kukamilika.

Rwanda imekua ikiwashtumu wakimbizi katika kambi hiyo kufanya maandamano yenye lengo la kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

Uhusiano kati ya Rwanda na DRC umekua ukidoora mara kwa mara kutokana na uhasama kati ya nchi hizi mbili. Lakini raia wa nchi hizo wamekua wakitembeleana bila kusumbuliwa kwenye mipaka.

Wakazi wa maeneo ya mipakani wamekua na ushirikiano wa karibu kutokana na hali hiyo ya kutembeleana.

Wadadisi wanasem auhasama kati ya nchi hizi mbili ni wa kisiasa na hauwezi kuwaathiri wananchi wa mataifa hayo mawili.

Bango hili linaonyesha njia ya kuingia kuelekea kambi ya wakimbizi wa DRC ya Kiziba, Rwanda, Septemba 6, 2016. STEPHANIE AGLIETTI / AFP