Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UN-USALAMA

Wafanyakazi 10 wa Umoja wa Mataifa watoweka Sudani Kusini

Umoja wa Mataifa unasema wafanyikazi 10 wa kutoa misaada hawajulikani walipo Kusini Magharib mwa hicho hiyo. Inaamika kuwa, wafanyakazi hao wametekwa wakiwa katika mji wa Yei.

Mdororo wa usalama waendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali Sudan Kusini.
Mdororo wa usalama waendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali Sudan Kusini. REUTERS/Stuart Price
Matangazo ya kibiashara

Hii sio mara ya kwanza kwa wafanyikazi wa kutoa misaada kutekwa nchini humo hasa wakati huu mzozo ukiendelea kushuhudiwa nchini humo kati ya wanajeshi wa serikali na waasi.

Hivi karibuni Makamu wa rais wa Sudan Kusini James Wani Igga aliwashtumu viongozi wa dini nchini humo kwa kuhubiri chuki dhidi ya serikali na kuchochea machafuko.

Igga amesema viongozi hao wamekuwa wakiwaambia raia wa taifa hilo kuwa, rais Kiir ni kiongozi mbaya matamashi ambayo amesema ni ya uchochezi.

Viongozi wa makanisa nchini Sudan Kusini wamekuwa wakimshutumu rais Kiir kwa kuendeleza vita nchini humo na kukataa kuheshimu mikataba ya amani kati yake na makundi ya waasi.

Machafuko nchini Sudani Kusini yamesababisha vifo vya watu wngi na maelfu wengine kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.