rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uhuru Kenyatta Raila Odinga Uchaguzi Kenya 2017

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenyatta na Odinga wawasihi Wakenya kufuatia uamuzi wao

media
Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamewasihi Wakenya kuwa uamuzi wao wa kusitisha tofauti zao haulengi uchaguzi wa mwaka 2022. TONY KARUMBA, SIMON MAINA / AFP

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamesema, uamuzi wao wa kusitisha tofauti zao za kisiasa haulengi uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.


Viongozi hao wawili wamesema lengo lao ni kuanzisha mwamko mpya wa kisiasa na kuwatumia wananchi wa taifa hilo.

Rais Kenyatta amesema anafahamu sio kila mmoja alifurahia maelewano yake na Odinga.

Kauli hii imekuja wakati huu, kukiwa na harakati za kuibadilisha Katiba ili kuanzishwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu mwenye mamlaka makubwa.

Kenya ilikumbwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia matokeo ya uchaguzi uliyorejelewa baada ya Mahakama kuu kubatilisha matokeo ya uchaguzi, ambapo Uhuru Kenyatta alikua aliibuka mshindi.

Katika uchaguzi mpya, matokeo yalionyesha kuwa Rais Kenyatta alimshinda mpinzani wake Raila Odinga, huku kiongozi huyo wa upinzani kufutilia mbali matokeo hayo, na hali hiyo kuzua hali ya sintofahamu nchini Kenya. Watu kadhaa walipoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa au kukamatwa.