rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tanzania Zanzibar

Imechapishwa • Imehaririwa

Tanzania yaadhimisha miaka 54 ya muungano

media
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akisalimiana na mke wa rais wa kwanza wa Zanzibar Bi Fatuma Karume wakati wa sherehe za miaka 53 ya muungano. April 26, 2017 Ikulu/Tanzania

Tanzania inaadhimisha Alhamisi wiki hii miaka 54 tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuunda taifa moja la Tanzania.


Tarehe 26 Aprili 1964, Tanganyika iliugana na Zanzibar na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maadhimisho ya mwaka huu yanayongozwa na rais John Pombe Magufuli mjini Dodoma, na yanafanyika wakati huu muungano huo ukiendelea kukumbwa na changamoto mbalimbali.

Mwanaharakati wa kwenye mitandao ya kijamii, mtanzania ambaye makaazi yake ni nchini Marekani Mange Kimambi amekua akiratibu maandamano kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiitisha maandamano nchi nzima dhidi ya rais Magufuli kwa kile anachodai kuwa amekuwa akikiuka haki za binaadam na kukandamiza uhuru wa kisiasa nchini Tanzania

Rais Magufuli alipiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa alipochukua hatamu ya uongozi wa nchi.Alisema uchaguzi umekwisha sasa ni wakati wa kuchapa kazi.

Hivi karibuni polisi iliahidi kuwaadhibu vikali wale watakao jaribu kuitikia wito wa kuandamana dhidi ya serikali.

Marekani na Uingereza wametoa wito kwa raia wao waishio nchini Tanzania kuwa waangalifu baada ya onyo hilo la polisi ya Tanzania.

Baadhi ya makamanda wa polisi walisisitiza kuwa wale ambao watathubutu kushiriki maandamano hayo watakiona "cha mtima kuni".

"Polisi inaweza (wakati wa maandamano Alhamisi wiki hii) kutumia mabomu ya machozi, "ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza imeonya, huku ikitoa wito kwa raia wa Uingereza waishio nchini Tanzania "kuwa makini "." Maandamano yaliyotangulia yalisababisha vifo. "

Mamlaka ya Uingereza ilipendekeza "kuepuka kuwa karibu na umati wa watu na maandamano", kuwa na "njia ya mawasiliano wakati wote" na kufuatilia maendeleo kupitia vyombo vya habari nchini humo. "

Siku ya Jumanne wiki hii, ubalozi wa Marekani ulitoa onyo kama hilo kwa raia wake waishio Tanzania".

Tayari watu saba wamekamatwa mjini Arusha nchini Tanzania wakihojiwa kuhusiana na majukumu yao katika maandamano ya kisiasa dhidi ya serikali mnamo tarehe 26 Aprili ambayo ni siku ya muungano.