rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Rwanda Kenya Burundi Tabia nchi

Imechapishwa • Imehaririwa

Mvua zinazonyesha zaua watu 18 Rwanda

media
Wanawake hawa wakifanya shughuli yao ya kilimo magharibi mwa Rwanda, Lakini wakulima wengi wamesema mvua zimeharibu mashamba yao. RFI/St├ęphanie Aglietti

Mvua kubwa imeendelea kunyesha katika mataufa ya Afrika Mashariki na Kati. Nchini Rwanda watu kumi na wanane wamepoteza maisha wiki hii, baada ya kusumbwa na maji.


Mbali na maaafa hayo, makaazi ya watu yameharibika hasa wale wanaoishi katika maeneo ya milima.

Nchini Kenya, hali imekuwa vivyo hivyo baada ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya mitaa ya jiji kuu Nairobi kama Buruburu kujaa maji.

Nchini Burundi, hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura, maeneo ya Maramvya, Carama na maeneo ya mabondeni ndio yameathrika zaidi na mvua hizo zinazoendelea kunyesha.

Wakulima kwa upande wao wanasema kuwa hawaamini kuwa msimu huu watapata mavuno ya kutosha.