rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uhuru Kenyatta Raila Odinga

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenyatta kuzindua rasmi kongamano la tano la magavana Kakamega

media
Rais Uhuru Kenyatta atazindua kongamano la magavana ambalo pia litahudhuriwa na kuhotubiwa na kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga. ┬ęSIMON MAINA/AFP

Kongamano la tano la Magavana wanaongoza serikali ya Kaunti nchini Kenya, linazinduliwa rasmi Jumanne wiki hii na rais Uhuru Kenyatta katika Kaunti ya Kakamega.


Miongoni mwa masuala muhimu yanayojadiliwa katika kongamano hilo ambalo pia litahudhuriwa na kuhotubiwa na kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, ni pamoja na hali ya Afya, Kilimo, Makaazi, Biashara na Miundo Mbinu.

Magavana 47, wawakilishi wa serikali kuu , wafadhili wa Kimataifa, wananchi na wadau wengine wanakutana tumia kuthathmini hatua zilizopigwa, changamoto zilizojitokeza kwa muda wa miaka mitano tangu kuanza kwa mfumo huo wa serikali nchini Kenya.

Hata hivyo, ufisadi na ukabila umeonekana kukithiri sana katika serikali mbalimbali za Kaunti kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Tume ya kupambana na ufisadi EACC.

Wizi wakati wa manunuzi na kutoa ajira kwa ukabila na upendeleo ni miongoni mwa masuala ambayo yanadaiwa kuongoza katika fedha zinazopatiwa katika serikali mbalimbali za Kaunti.

Magavana wamekuwa wakikanusha madai hayo na kusema kutaka serikali kuu kuongeza kiwango cha fedha inayotoa kwa serikali za Kaunti.

Magavana wanasema kwa sasa fedha hizo hazitoshi na sasa inataka kiasi hicho kuongezeka hadi asilimia 45.

Wakenya walipata Katiba mpya mwaka 2010, iliyounda serikali za Kaunti zinazoongozwa na Magavana huku lengo kubwa likiwa ni kuwapa nafasi wananchi kufanya maamuzi ya maendeleo na uongozi katika maeneo wanayotokea.