Pata taarifa kuu
KENYA-MAGAVANA-UONGOZI

Magavana nchini Kenya wakutana kujadili mafanikio na changamoto baada ya miaka mitano

Kongamano la tano la Magavana wanaongoza serikali ya Kaunti nchini Kenya, linafanyika wiki hii  katika Kaunti ya Kakamega, Magharibi mwa nchi hiyo kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.

Kongamano la Magavana nchini Kenya lililofanyika mwaka 2017
Kongamano la Magavana nchini Kenya lililofanyika mwaka 2017 http://devolution.cog.go.ke/#
Matangazo ya kibiashara

Magavana 47, wawakilishi wa serikali kuu , wafadhili wa Kimataifa, wananchi na  wadau wengine wanakutana tumia kuthathmini hatua zilizopigwa, changamoto zilizojitokeza kwa muda wa miaka mitano tangu kuanza kwa mfumo huo wa serikali nchini Kenya.

Wakenya walipata Katiba mpya mwaka 2010, iliyounda serikali za Kaunti zinazoongozwa na Magavana huku lengo kubwa likiwa ni kuwapa nafasi wananchi kufanya maamuzi ya maendeleo na uongozi katika maeneo wanayotokea.

Miongoni mwa masuala muhimu yanayojadiliwa katika kongamano hilo ambalo pia litahudhuriwa na kuhotubiwa na rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, ni pamoja na hali ya Afya, Kilimo, Makaazi, Biashara na Miundo Mbinu.

Mafanikio yaliyoonekana tangu kuwepo kwa serikali za Kaunti ni kuimarika kwa miundo mbinu hasa barabara katika maeneo ya Mandera, Garrisa na Lodwar ambayo yamekosa barabara za lami tangu historia ya nchi hiyo mwaka 1963.

Hata hivyo, ufisadi na ukabila umeonekana kukithiri sana katika serikali mbalimbali za Kaunti kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Tume ya kupambana na ufisadi EACC.

Wizi wakati wa manunuzi na kutoa ajira kwa ukabila na upendeleo ni miongoni mwa masuala ambayo yanadaiwa kuongoza katika fedha zinazopatiwa katika serikali mbalimbali za Kaunti.

Hata hivyo, Magavana wamekuwa wakikanusha madai hayo na kusema kutaka serikali kuu kuongeza kiwango cha fedha inayotoa kwa serikali za Kaunti.

Katiba inaeleza kuwa, kati ya mapato yote ya serikali kuu kila mwaka, ni lazima itume asilimia 15 kwa serikali za Kaunti kwa ajili ya maendeleo.

Magavana wanasema kwa sasa fedha hizo kwa sasa hazitoshi na sasa inataka kiasi hicho kuongezeka hadi asilimia 45.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.