rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Afrika Tanzania

Imechapishwa • Imehaririwa

Wafanyabiashara wa Ufaransa Wabaini fursa za uwekezaji Tanzania

media
Balozi wa Uswis nchini Tanzania Florence Mattli (kushoto), balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier (katikati) na balozi msaidizi wa Canada Susan Steffan, 14 Machi 2018 Emmanuel Makundi/RFIKiswahili

Serikali ya Tanzania imewataka wawekezaji kutoka nchini Ufaransa kuwekeza katika viwanda vya bidhaa za kilimo pamoja na kuangazia soko la bidhaa mbalimbali za vyakula nchini Ufaransa ili kukuza mashirikiano ya kibiashara baina ya nchi hizo mbili


Akizungumza wakati ujumbe wa sekta binafsi kutoka nchini Ufaransa MEDEF ukihitimisha ziara ya siku tatu ya kuangalia fursa za uwekezaji nchini humo, Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Dkt.Charles Mwijage amesema Ufaransa imefanikiwa katika biashara Duniani kuja nchini Tanzania ni fursa adhim kutokana na kuwa na maeneo mbalimbali ya uwekezaji.

Silvester Koka ni Mfanyabiashara nchini humo amesema Wawekezaji hao wameamua kuwekeza katika kiwanda cha uzalishaji wa Unga wa Muhogo katika mkoa wa Lindi kusini mwa Tanzania

MEDEF wamekutana na Taasis ya Sekta Binafsi nchini na kuangazia maeneo muhimu ya kushirikiana, Dakta Reginald Mengi ni Mwenyekiti wa TPSF anasema Tanzania ina kila ni fursa ya uwekezaji ni wakati wa wafanyabiashara kuneemeka.

  "Tanzania ina ardhi,ina madini kama tukiamua kulima mazao ya kibiashara tutanufaika kwani ardhi yetu ina rutuba ukilinganisha na mataifa mengi ya ulaya" alisema Dakta Mengi

Akizungumzia Fursa za kibiashara nchini Ufaransa John Mwakisambe ambae anaishi nchini humo amesema soko la asali pamoja na unga lipo ingawaje wafanyabiashara wa Tanzania wanashindwa kukidhi soko kutokana na vifungashio duni vuya bidhaa zao

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier anaselengo serikali yake inaona Tanzania ni kitovu cha kibiashara barani Afrika kutoka na nchi hiyo kuwa kati kati ya jumuiya ya SADC na EAC

"Tanzania inazikutanisha nchi nyingi kwa hivyo ni muhimu kuweka mashirikiano ya kibiashara ili kulikamata soko la Afrika" alisema Clavier

Ripoti ya Mwandishi wa RFI Kiswahili,Steven Mumbi