rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Kenya Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenya yaomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe Kenneth Matiba

media
Keneth Matiba, mwanasiasa mkongwe nchini Kenya siku za uhai wake nairobinews.

Wakenya wanaomboleza kifo cha Kenneth Matiba, mwanasiasa mkongwe aliyekuwa katika mstari wa mbele kupigania kuwepo kwa vyama vingi na ukombozi wa pili wa nchi hiyo.


Matiba amefariki dunia akiwa na miaka 85 baada ya kuugua muda mrefu kutokana na kiharusi alichopata wakati akiwa mfungwa wa kisiasa miaka ya 90, kabla ya kuachiliwa huru.

Kifo chake kimetangazwa na rais Uhuru Kenyatta ambaye amemwelezea kama mwanasiasa aliyepigia demokrasia nchini humo.

“Kenya imepoteza mmoja wa mtoto wake aliyepigania demokrasia tunayofurahia,” alisema Kenyatta.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa waliofungwa naye kutokana na harakati za kutaka vyama vingi, wameishtumu serikali kwa kushindwa kumsaidia mwanasiasa huyo aliyefilisika wakati alipohitaji msaada.

Mbali na kuwa mwanasiasa, alikuwa mfanyibiashara akimiliki hoteli kadhaa za kitalii lakini biashara zake ziliporomoka.

Aliwahi pia kuwa kiongozi wa soka nchini humo.

Mbali na nyadhifa hizo, aliwahi kuwa Waziri katika serikali ya rais mustaafu Moi.

Aliwania urais mwaka 1992 na kumaliza wa pili, matokeo ambayo aliyakataa na kusema aliibiwa kura na aliyekuwa mshindi Daniel Arap Moi.