Pata taarifa kuu
UGANDA-MITANDAO YA KIJAMII-KODI

Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Uganda kutozwa kodi

Uganda inapanga kuwatoza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii kila siku, kuanzia mwezi Julai.

Mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Fedha Matia Kasaija ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kuwa, hatua hii inalenga kuisadia serikali kukusanya mapato.

“Tunahitaji fedha za kuisaidia kuimarisha usalama, kuweka miundo mbinu ya umeme na mambo mengine muhimu,” alisema.

Hata hivyo, wanaharakati wamepinga mpango huu kwa kile wanachosema ni mpango wa serikali ya rais Yoweri Museveni kuminya uhuru wa kujieleza.

Watumiaji wanatarajiwa kutozwa Shilingi za Uganda 200 au 100.

Mapema mwezi huu, rais Yoweri Museveni alimwandikia barua Waziri Kasaija na kumwagiza kuja na mbinu za kukusanya fedha kutoka watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Museveni ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30 sasa amesema Mamilioni ya raia wa Uganda wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kusambaza habari za uongo.

Hata hivyo, mpango huu hautawaathiri wanaotumia mitandao hiyo kwa ajili ya masuala ya elimu.

Wanasiasa wa upinzani pia wamesema hiyo ni njia ya rais Museveni kuonesha kuwa anaongopa ushawishi wa mitandao ya kijamii kama facebook na Twitter.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.