rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya EAC William Ruto Mazingira

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenya: Bei ya mkaa juu wakati huu wataalamu wakionya kuhusu ukataji miti

media
Biashara ni moja ya biashara kuu ya wananchi wa kipato cha chini barani Afrika LA Bagnetto

Bei ya mkaa imeongezeka maradufu nchini Kenya na kuwaathiri watu wenye kipato kidogo ambao ndio watumiaji wakubwa wa mkaa wa majumbani, hatua inayotokana na zuio la Serikali kuhusu biashara ya uchomaji mkaa nchini Kenya.


Taarifa za hivi karibuni kuhusu bei ya mkaa zinaonesha kuwa mfuko mdogo wa mkaa unauzwa kwa kati ya shilingi 2500 za kenya kutoka shilingi 1500 wiki tatu zilizopita, hatua inayotokana na zuuo na miezi mitatu lililotolewa na Serikali kuhusu ukataji miti kwaajili ya uchomaji wa mkaa.

Naibu wa rais William Ruto akizungumza Februaru 24 mwaka huu alitangaza Serikali kupiga marufuku uvunaji wa miti kwenye misitu ya Serikali na kumuagiza waziri wa mazingira Keriako Tobiko kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu tatizo la ukaukaji wa miti.

Kilo nne ya mkaa wa majumbani hivi sasa unauzwa kati ya shilingi 120 kutoka shilingi 70 mwezi uliopita.

Jijini Nairobu wanunuzi wanalazimika kununua gunia zima la mkaa huku bei zikipanda maradufu kwenye miji ya Nakuru na Chemlil.

Bei ya mkaa imeongeza mara mbili zaidi tangu mwaka 2008 hali iliyowafanya watu wa kipato cha chini kuingia gharama zaidi.

Serikali ya Kenya inasema kasi ya ukataji misitu kwaajili ya uchomaji wa mkaa imeathiri kwa kiwango kikubwa unyeshaji wa mvua na kusababisha ukame kwenye maeneo mengi ya nchi ikiwa ni pamoja na mito kukauka.

Mataifa mengi ya ukanda wa Afrika Mashariki yanakabiliwa na tatizo la ukame linalotokana na biashara ya mkaa ambayo inahusisha ukataji mkubwa wa miti, hali ambayo wataalamu wanasema imesababisha mabadiliko ya tabia nchi yanayoshuhudiwa kwa sasa duniani.

Licha ya kampeni mbalimbali zilizoanzishwa kwenye nchi wanachama za Afrika Mashariki kuhusu upandaji wa miti na kutoharibu misitu, wananchi wengi wa kipato cha chini wamekuwa wakijihusisha na biashara ya mkaa na kuathiri pakubwa mazingira.