Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-NASA

Mvutano watishia kuuvunja muungano wa NASA

Viongozi wawili wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wamesema hawaungi mkono kitendo cha cha ODM kinachounda muungano huo, kumwandikia barua spika wa Senate kumweleza kiongozi wa walio wachache Moses Wetang'ula ameondolewa katika nafasi hiyo.

Moses Wetangula  mmoja wa viongozi wa NASA na kiongozi wa walio wachache katika bunge la Senate
Moses Wetangula mmoja wa viongozi wa NASA na kiongozi wa walio wachache katika bunge la Senate Reuters/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka, wamekutana na Wentangula ambaye ni kiongozi wa chama cha FORD Kenya na kupinga hatua iliyochukuliwa na chama cha ODM kinachoongozwa na kiongozi wa muungano huo Raila Odinga.

Mudavadi na Wetangula wamesema wanamuunga mkono Wetang'ula na wanaendelea kumwamini kama kiongozi wa walio wachache katika bunge hilo la Senate.

Siku ya Alhamisi, chama cha ODM kilicho na Maseneta wengi kilimwandikia Spika Ken Lusaka na kumwarifu kuwa uongozi wa walio wachache umechukuliwa na Seneta kutoka chama chao, Seneta James Orengo.

Wetang'ula amekasirishwa na hatua ya chama cha ODM na kusema kuwa hataondoka katika nafasi hiyo.

“Iwapo mnataka talaka, lazima kutakuwa na kelele na mvutano mkali na haitakuwa rahisi kuniondoa,” alisema Seneta Wetangu'la

Maendeleo haya yanatishia umoja ndani ya muungano huo wa NASA.

Hata hivyo, haitakuwa rahisi iwapo vyama vya Wiper, ANC na FORD Kenya vitaendelea kuwa pamoja kwa sababu, mkataba uliounda muungano huo, unasema mvutano huo unaweza kuvunjika tu iwapo vyama vitatu vitajiondoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.