rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uhuru Kenyatta

Imechapishwa • Imehaririwa

Mafuriko yasababisha vifo vya watu 15 nchini Kenya

media
Hali ya mafuriko jijini Nairobi, mkaazi huyu aliamua kutumia njia ya kipekee kuepuka maji mengi katika barabara ya Moi Avenue twitter.com/hashtag/nairobifloods

Watu 15 wamepoteza maisha nchini Kenya kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.


Ripoti zinasema kwa muda wa siku mbili zilizopita, mvua hiyo ilisababisha mafuriko makubwa jijini Nairobi na maeneo mengine ya nchi hiyo.

Wakenya wamekuwa wakihesabu hasara na kuomboleza vifo vya watu hao waliosombwa na maji katika Kaunti za Nairobi, Pwani, Mashariki na Kaskazini Mashariki.

Miili ya watu wanne, imepatikana katika mto Athi pembezoni mwa barabara kuu kutoka jiji kuu Nairobi kwenda Kangundo.

Mafuriko makubwa yaliyotokea baada ya mvua ya siku ya Alhamisi, yamesababisha kuharibiwa kwa miundo mbinu kama barabara na madaraja.

Katika Kaunti ya Taita Taveta, watoto wawili walio na miaka mitano na minane ni miongoni mwa watu walipoteza maisha baada ya kuzama majini.

Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo, imeendelea kutoa tahadhari ya kutokea kwa mvua na mafuriko zaidi katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Wito umetolewa kwa maeneo ambayo yataendelea kupokea mvua, kuhamia katika maeneo yaliyoinuka na kuacha kutembea kwenye maji yaliyosimama.