Pata taarifa kuu
UGANDA-HAKI ZA WANAWAKE-BUNGE

Mbunge wa Uganda aliyetaka wanawake kupewa adhabu ya kupigwa aomba radhi

Mbunge nchini Uganda Onesmus Twinamasiko, ameomba radhi baada ya hivi karibuni kutoa kauli tata ya kuwahimiza wanaume kuwapiga wake zao kama njia ya kuwafunza nidhamu.

Mbunge wa Uganda Onesmus Twinamasiko aliyewahimiza wanaume kuwapiga wake zao kama njia ya kuwafunza nidhamu
Mbunge wa Uganda Onesmus Twinamasiko aliyewahimiza wanaume kuwapiga wake zao kama njia ya kuwafunza nidhamu twitter.com/ntvuganda
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya mbunge huyo, iliyoshtumiwa vikali na makundi ya wanaharakati wa wanawake na watetezi wa haki za binadamu, waliomtaka kuomba radhi.

Mbunge huyo ameliandikia barua bunge na kusema kuwa naomba radhi kwa matamshi hayo na kusisitiza kuwa haungi mkono kupigwa kwa wanawake.

“Naomba mkubali na mnisamehe kwa matamshi niliyoyatoa, yaliyowakera wananchi wa Uganda na hasa wanawake,” aliandika Twinamasiko katika barua yake.

Twinamasiko alinukuliwa wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni NTV, aliposema  mwanamume ni lazima ampe nidhamu mkewe kwa kumpiga kidogo.

“Kama mwanamume unahitaji kumpa adhabu mke wako, mpige kidogo, mwangushe kama njia ya kumyoosha " kauli tata aliyotoa wakati wa siku ya Kimataifa ya wanawake duniani.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge wamekataa kukubali ombi lake kwa kile wanachosema kuwa hakuwa mkweli na hakumaanisha alichokisema katika barua hiyo.

Ripoti ya serikali mwaka 2016 inaonesha kuwa mwanamke mmoja kati ya watano kati ya umri wa miaka 14 na 49 wanapigwa au kudhulumiwa kimapenzi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.